Skip to main content

Kutuhusu

Je, California Mosaic Small Business Center ni nini?

California Mosaic Small Business Center ni mradi wa shirika la International Rescue Committee wa kusaidia wafanyabiashara wahamiaji 880,000 wa California kupata mafunzo na usaidizi wa kiufundi kuhusu biashara kwa lugha zao. Mpango huu umefadhiliwa kupitia Ruzuku iliyotolewa na Ofisi ya California Inayosimamia Masuala ya Biashara Ndogo.

Sehemu kuu za Mpango huu zinajumuisha:

  • Tovuti yenye lugha mbalimbali (Kiarabu, Kidari, Kipashto, Kiswahili, Kihispania na Kifaransa) inayowahudumia wafanyabiashara wote wa California, popote walipo
  • Wataalam wa kibiashara wanaotoa mafunzo kwa wamiliki wa biashara ndogo kwa kuangazia mada anuwai
  • Vikundi vya lugha mbalimbali na warsha za mafunzo ya ana kwa ana katika Vituo na mtandaoni, zinazopatikana kwenye tovuti ya California Mosaic Small Business Center, kuhusu mada kama vile upangaji wa biashara, utangazaji, uendeshaji wa biashara, udhibiti wa fedha, uagizaji/uuzaji nje, na zaidi
  • Huduma za kifedha kupitia ukaguzi na kupendekezwa kwa wakopeshaji wa kijamii ili kupata mikopo ya biashara, pamoja na kupendekezwa kwa wataalam wa fedha wa IRC na huduma za msingi utoaji mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wanaohitaji mikopo na ustawi wa kifedha

 

irc_horizontal_lockup_rgb 1.png

Kuhusu Shirika la International Rescue Committee

Shirika la International Rescue Committee (IRC) huwasaidia waathiriwa wa majanga—ikiwa ni pamoja na janga la mabadiliko ya tabianchi—kuokoa maisha, kupata afueni na kuendeleza maisha yao. Msingi wa shirika hili ni wito wa Albert Einstein mwaka wa 1933, IRC sasa inafanya kazi katika zaidi ya nchi 40 zilizoathiriwa na majanga na pia kote Ulaya na Amerika. Tunaleta suluhu ya kudumu kwa kutoa huduma za afya, kuwasaidia watoto kupata elimu, na kuwawezesha watu binafsi na jamii kujitegemea, kila mara tukijitahidi kushughulikia ubaguzi unaowakabili wanawake na wasichana

 

osba_logo_final_for_light_bkgd_1.png

Kuhusu Ofisi ya California Inayosimamia Masuala ya Biashara Ndogo

Ofisi ya California Inayosimamia Masuala ya Biashara Ndogo (CalOSBA) huchangia ukuaji na uvumbuzi wa kiuchumi na hutoa habari na usaidizi kwa biashara ZOTE ndogo au zinazoanza huko California ili kuziwezesha kuzingatia kanuni husika, kunufaika na mipango iliyopo na kutumia rasilimali ipasavyo. CalOSBA hutetea biashara ndogo, kwa kuwakilisha maoni na maslahi yao katika jimbo lote na kutetea ufikiaji sawa wa mitaji, soko na mitandao ili kuwawezesha wamiliki wote wa biashara ndogo California kuanzisha, kudhibiti na kukuza biashara zao.